Swahili New Testament Bible

Acts 16

Acts

Return to Index

Chapter 17

1

 

 Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia, walisafiri mpaka Thesalonika ambako kulikuwa na sunagogi la Wayahudi. 

 


2

 

 Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akatumia Maandiko Matakatifu. 

 


3

 

 Aliyaeleza na kuonyesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka wafu. Akawaambia, "Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo." 

 


4

 

 Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa tabaka la juu, walijiunga nao. 

 


5

 

 Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni, wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani. 

 


6

 

 Lakini hawakuwapata na hivyo walimburuta Yasoni pamoja na ndugu wengine mpaka kwa wakuu wa mji, wakapiga kelele: "Watu hawa wamekuwa wakivuruga dunia yote na sasa wako hapa mjini. 

 


7

 

 Yasoni amewakaribisha nyumbani kwake. Wote wanafanya kinyume cha amri ya Kaisari wakisema eti `Kuna mfalme mwingine aitwaye Yesu."` 

 


8

 

 Kwa maneno hayo waliwatia wasiwasi wakuu wa mji na kundi la watu. 

 


9

 

 Wakawafanya Yasoni na wenzake watoe dhamana, kisha wakawaacha waende zao. 

 


10

 

 Usiku, wale ndugu waliwahimiza Paulo na Sila waende Berea. Mara tu walipofika huko, walikwenda katika sunagogi la Wayahudi. 

 


11

 

 Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonika. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli. 

 


12

 

 Wengi wao waliamini na pia wanawake wa Kigiriki wa tabaka la juu na wanaume pia. 

 


13

 

 Lakini, Wayahudi wa Thesalonika walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu. 

 


14

 

 Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea. 

 


15

 

 Wale ndugu waliomsindikiza Paulo walikwenda pamoja naye mpaka Athene. Kisha, wakarudi pamoja na maagizo kutoka kwa Paulo kwamba Sila na Timotheo wamfuate upesi iwezekanavyo. 

 


16

 

 Paulo alipokuwa anawasubiri Sila na Timotheo huko Athene, moyo wake ulighadhibika sana alipoona jinsi mji huo ulivyokuwa umejaa sanamu za miungu. 

 


17

 

 Alijadiliana na Wayahudi na watu wengine waliomcha Mungu katika sunagogi; na kila siku alikuwa na majadiliano sokoni pamoja na wowote wale waliojitokeza. 

 


18

 

 Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, "Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?" Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, "Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni." 

 


19

 

 Hivyo walimchukua Paulo, wakampeleka Areopago, wakasema, "Tunataka kujua jambo hili jipya ulilokuwa unazungumzia. 

 


20

 

 Vitu vingine tulivyosikia kwa masikio yetu vinaonekana kuwa viroja kwetu. Tungependa kujua mambo haya yana maana gani." 

 


21

 

 Wananchi wa Athene na wakazi wengine wa huko walikuwa wanatumia wakati wao wote kuhadithiana na kusikiliza habari mpyampya. ic 

 


22

 

 Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema, "Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba ninyi, kwa vyovyote, ni watu wa dini sana. 

 


23

 

 Sababu yenyewe ni kwamba katika pitapita yangu niliangalia sanamu zenu za ibada nikakuta madhabahu moja ambayo imeandikwa: `Kwa ajili ya Mungu yule Asiyejulikana.` Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye ninayemhubiri kwenu. 

 


24

 

 Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na nchi; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu. 

 


25

 

 Wala hatumikiwi kwa mikono ya watu kana kwamba anahitaji chochote kile, kwa maana yeye mwenyewe ndiye anayewapa watu uhai, anawawezesha kupumua na anawapa kila kitu. 

 


26

 

 Kutokana na mtu mmoja aliumba mataifa yote na kuyawezesha kuishi duniani kote. Aliamua na kupanga kabla kabisa lini na wapi mataifa hayo yangeishi. 

 


27

 

 Alifanya hivyo, ili mataifa hayo yapate kumfuata, na kama vile kwa kupapasapapasa, yapate kumfikia. Hata hivyo lakini, Mungu hayuko mbali na kila mmoja wetu. 

 


28

 

 Kama alivyosema mtu mmoja: `Ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu, na tuko!` Ni kama washairi wenu wengine walivyosema: `Sisi ni watoto wake.` 

 


29

 

 Ikiwa basi, sisi ni watoto wa Mungu, haifai kumfikiria Mungu kuwa kama dhahabu, fedha au hata jiwe lililochongwa na kutiwa nakshi na binadamu. 

 


30

 

 Mungu alifanya kama kwamba haoni nyakati zile watu walipokuwa wajinga. Lakini sasa, anaamuru watu wote kila mahali watubu. 

 


31

 

 Kwa maana amekwisha weka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki kwa njia ya mtu mmoja aliyemteua. Mungu amewathibitishia wote jambo hili kwa kumfufua mtu huyo kutoka wafu!" 

 


32

 

 Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo la kufufuka kwa wafu, wengine wao waliangua kicheko; lakini wengine walisema, "Tunataka kukusikia tena juu ya jambo hili!" 

 


33

 

 Hivyo, Paulo aliwaacha, akatoka barazani. 

 


34

 

 Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, mwanamke mmoja aitwaye Damari na wengineo. 

 


Acts 18

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: